Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 

 kuoa ili kuondoa nuksi ?....Ha Ha Habari ndio hii (Hiyo)

Go down 
AuthorMessage
rekesheiPosts : 17
Join date : 2008-06-20

kuoa ili kuondoa nuksi ?....Ha Ha Habari ndio hii (Hiyo) Empty
PostSubject: kuoa ili kuondoa nuksi ?....Ha Ha Habari ndio hii (Hiyo)   kuoa ili kuondoa nuksi ?....Ha Ha Habari ndio hii (Hiyo) I_icon_minitimeSun Jun 29, 2008 10:38 am

Mpenzi msomaji, lipo jambo moja limenivutia kukumegea leo kuhusu ndoa za siku hizi. Huko tulikotoka kuolewa au kuoa lilikuwa ni tukio la baraka. Lakini siku hizi hali ikoje?

Liko tukio moja nililosimuliwa kutoka huko Moshi mkoaniKilimanjaro ambapo dada mmoja aliolewa siku ya Jumamosi, lakini siku mbili baadaye, yaani Jumanne akamwacha yule bwana na kutokomea kwa mwanaume mwingine. Kisa ni nini?

Msimulizi wa tukio hili anasema kuwa dada huyo japokuwa alikuwa na mchumba huyo waliyefunga naye ndoa, lakini hakuwa anampenda kwa dhati bali alikuwepo mwingine wa ubani, tena mume wa mtu aliyemzibua kimapenzi.

Kwa maelezo ya bibie eti mchumba yule hakumpenda ila alitaka afunge naye ndoa ili kuondoa nuksi na iwe kwenye kumbukumbu kwamba hata yeye aliwahi kuoewa kwa ndoa takatifu.

Mashuhuda wa harusi wa bibie huyo wanasema ndoa ilikuwa ya gharama kubwa na iliyofana lakini walishangazwa na taarifa kuwa ndoa imesambaratika na bibie kaenda kwa mshikaji wake ambaye ni mume wa mtu.

Inasemekana ndugu wa bwana harusi wamecharuka na kuapa kumrudisha bibi harusi kwa mumewe kwa gharama zozote zile. Na kwamba shugadadi huyo anayemzingua shemeji yao naye atakiona cha mtema kuni.

Hata hivyo, habari zingine zinadai kuwa bibie katu hatamrejea mumewe kwa kile alichodai, kwanza alitaka tu aolewe ndoa kuondoa nuksi na pili aliyemuoa hamridhishi kimapenzi.

Mpenzi msomaji, hayo ndiyo mambo na hakika maisha ndivyo yalivyo. Eti siku hizi kuolewa ni fasheni ya kuondoa nuksi.

Wiki hii nilipata wasaa kusikiliza kipindi cha Longa mwanamume kwenye kituo cha televisheni cha ITV kikihusu baadhi ya kinamama kuwaachia watumishi wa nyumbani kufanya kazi ambazo zingepaswa kufanywa na wao.

Mfano, kumpokea baba arudipo kazini, kumwandalia baba chakula, kumwekea maji bafuni na hata kutandika kitanda. Eti kazi hizi zote alipaswa kuzifanya mama ili kumwepushia baba vishawishi vya kummezea mate housigeli.

Nilipogusia jambo hili katika kikao Fulani na marafiki zangu juzi, mmoja akasema; ``Kinamama wengine wako katika nyumba zao tu kuweka rekodi kuwa wameolewa, lakini mapenzi hakuna``.

Mwingine akamdakia; ``wewe hujui ukiona hivyo ujue vituko vya mumewe vimemfika kooni. Pengine anapewa taarifa zake (mume) kuhusu nyendo zake za kihuni huko nje, au mume yule hamjali tena kama mwanzoni walipooana na kadhalika``.

Mwingine akapigilia msumari kwa kusema; ``katika nyumba nyingine ukiona mama hajali kumhudumia mumewe nyumbani, basi ujue anaye mshikaji nje ya ndoa anayemzingua hivyo mume si chochote.

Bibie niliyemzungumzia mwanzoni mwa makala hii yeye hakutaka aone vurugu za ndoa ndio sababu akaamua kujiengua mapema na kwenda kumuegemea shugadadi wake.

Lakini swali ni je, haya ndiyo maisha tunayotaka? Hizi fasheni za maisha eti kuondoa nuksi zinatoka wapi?

Je, huku ni kuondoa nuksi au ni kuharibiana kimaisha?

Kwa ujumla yule mama anayempiga chenga mumewe ndani na kuchepuka kwa bwana wa pembeni, sidhani ana amani yoyote rohoni mwake.

Hali kadhalika yule bibie aliyemtosa mumewe wa ndoa muda mfupi na kukimbilia kwa mume wa mtu, bado atapata vikwazo na vishawishi vya kusaka mabwana wengine.

Kama hukutosheka na mmoja ndio utatosheka na wanaume wengine lukuki? Upo msemo mmoja wa mtaani usemao ``Nimezunguka bucha zote lakini nyama ni ile ile``.

Hii ikimaanisha kuwa kile baadhi ya kinamama wanachokimbia kwenye nyumba zao ndio hicho hicho watakikuta kule waendako.

Mpenzi msomaji, kinachotakiwa ni watu kuheshimu nyumba zao. Mke au mume ulimtupia jicho mwenyewe, ukampenda sasa wamtilia shaka ya nini? Si maji uliyavulia nguo, sasa kwa nini uogope kuyaoga? Hakika Maisha Ndivyo Yalivyo.

Kuolewa ni baraka toka kwa Mwenyezi Mungu siyo fasheni wala kuondoa nuksi kama baadhi yetu wanavyodai.

Hata mababu zetu walifurahia sana ndoa na zilidumu tofauti na sasa ambapo tukio hilo linapewa uzito mdogo.

Siyo siri kuwa baadhi ya watu wanaoa au kuolewa lakini wanajenga au wanaendeleza mahusiano ya nje ya ndoa.

Raha gani wanapata huko, wahusika wanajua. Faida gani wanapa ndio pamoja na maambukizi ya magonjwa hatari kama Ukimwi. Habari ndiyo hiyo.
Back to top Go down
View user profile
 
kuoa ili kuondoa nuksi ?....Ha Ha Habari ndio hii (Hiyo)
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: Your first category :: MAPENZI NA MAONGEZI-
Jump to: