Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 

 CHADEMA inapoanza kubomoka na kupoteza umaarufu wake

Go down 
AuthorMessage
pedejeePosts : 9
Join date : 2008-07-02

CHADEMA inapoanza kubomoka na kupoteza umaarufu wake Empty
PostSubject: CHADEMA inapoanza kubomoka na kupoteza umaarufu wake   CHADEMA inapoanza kubomoka na kupoteza umaarufu wake I_icon_minitimeWed Jul 02, 2008 3:55 pm

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemsimamisha uongozi Makamu Mwenyekiti wake, Bw. Chacha Wangwe kwa madai ya kukiuka kanuni taratibu na Katiba ya chama hicho.

Hata hivyo, Bw. Wangwe ameiambia Nipashe kwamba hajui kosa lake, lakini anapinga hatua hiyo aliyoiita si mgogoro kama wengi wanavyoweza kuiona bali ni `mchakato` ambao unaweza kuwa muhimu katika chama chao.

Hatua ya kumsimamisha Bw. Wangwe imechukuliwa baada ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho kilichokutana juzi, Juni 28 mwaka huu mjini Dodoma.

Kikao hicho kilidumu kwa zaidi ya saa 18 na kilimalizika saa 9:00 usiku.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwanasheria wa Chama hicho, Bw. Tundu Lissu alisema sababu ya kumvua uongozi Bw. Wangwe inatokana na kushindwa kuwasilisha hoja zake katika vikao husika na badala yake kutumia vyombo vya habari.

Alisema Bw. Wangwe amekuwa akivujisha taarifa mbali mbali zinazoamriwa na chama katika vikao vyake nyeti.

Bw. Lissu alisema Wangwe alisimamishwa baada ya wajumbe 24 kati ya 30 kumpigia kura ya siri ya kutokuwa na imani naye.

``Huu ni uamuzi mzito na ambao haujawahi kufanywa katika historia ya miaka 16 ya CHADEMA... Tunapenda kuwafahamisha wananchi wetu kwamba uamuzi huu mzito ulichukuliwa baada ya mjadala na tafakuri ya muda mrefu,`` alisema.

Aliongeza kuwa Kamati Kuu ya chama hicho ilifikia hatua hiyo dhidi ya Bw. Wangwe baada ya kuridhika na ushahidi kwamba amekiuka maadili ya uongozi na hivyo kupoteza sifa za kuendelea kuwa kiongozi wa Kitaifa wa CHADEMA.

Alizitaja sababu hizo kuwa ni pamoja na kujihusisha na kushiriki katika vikundi, vitendo vya uchonganishi na kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama na wanachama wake.

Alisema Wangwe amekuwa akijihusisha na kushirikiana na kikundi cha waliokuwa viongozi wa chama wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambao walifutwa uongozi na vikao halali vya chama na kwa kufuata Katiba na kanuni za chama.

Alifafanua kuwa Bw. Wangwe amekuwa akishiriki kuandaa, kufadhili na kushiriki katika mikutano ya siri kwa lengo la kuendeleza migogoro na hujuma kwa chama.

Alisema mikutano hiyo ilifanyika Ndugumbi, Dar es Salaam na pia Mwanza na ilimshirikisha pia Dk. Amani Walid Kabourou aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa (Bara), kabla hajahamia Chama cha Mapinduzi.

Dk. Kabourou alihamia CCM mara tu baada ya kushindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini.

``Kitendo cha kuandaa, kushiriki na kufadhili mikutano ya siri ya watu ambao wamechukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama, na ambao wamekihama chama baada ya kupoteza ridhaa ya kuwaongoza wananchi, kina tafisiri moja tu ya msingi: Kuendeleza migogoro na hujuma dhidi ya chama kwa lengo la kukidhoofisha na kukifanya kishindwe kuendeleza vita kubwa dhidi ya ufisadi uliojikita ndani ya Serikali na CCM ambayo imekipatia chama chetu sifa kubwa na uhalali kwa watanzania,`` alisema.

Alisema vitendo hivyo vinapingana moja kwa moja na maadili ya viongozi wa chama kama yalivyoelezwa katika sura ya kumi ya Katiba, Kanuni, Maadili na Itifaki za CHADEMA.

Pia Bw. Wangwe amedaiwa kutoa tuhuma nzito lakini zisizokuwa na msingi dhidi ya viongozi wenzake wa Kitaifa na watendaji wa chama bila kupitia vikao halali na wala kuzingatia taratibu za chama.

Bw. Tundu aliongeza kuwa Bw. Wangwe aidha moja kwa moja ama kwa kuwatumia viongozi na wanachama walioadhibiwa na vikao halali vya chama, amekuwa akiwatuhumu viongozi na watendaji wa chama kwa mambo ya uzushi na yasiyokuwa na ukweli na msingi wowote.

``Yeye mwenyewe amekuwa akisambaza uzushi kwamba kuna ufujaji na matumizi mabaya ya fedha za chama ambayo amekuwa akidai unafanywa na viongozi wa kitaifa, hususan Mwenyekiti wa chama Taifa na Katibu Mkuu na watendaji wa Makao Makuu ya chama,`` alisema.

Kadhalika, alisema amekuwa akisambaza uzushi kwamba viongozi wenzake wa kitaifa na watendaji Makao Makuu, wamekuwa wakikataa ruzuku ya chama kupelekwa mikoani na wilayani, na badala yake wamekuwa wakiitumia ruzuku hiyo kwa shughuli za Makao Makuu na kwa manufaa yao binafsi.

``Uzushi huu umetolewa licha ya Kamati Kuu ya chama ambayo, Bw. Chacha Wangwe alikuwa ni mjumbe kupokea na kupitisha taarifa zote zinazohusiana na mapato na matumizi ya fedha za chama na licha ya chama kutoa ruzuku ya vifaa na fedha taslimu tangu Mwaka 2006, kabla hata ya yeye kuchaguliwa kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA tarehe 17 Desemba Mwaka 2007.

Aidha, alisema hakuna hata kiongozi mmoja wa chama hicho akiwemo yeye mwenyewe (Wangwe) hawajapokea hata senti moja ya fedha za chama kama posho au mishahara.

``Tuhuma hizi za uzushi na uongo juu ya kuwepo ufujaji na matumizi mabaya ya fedha za chama, zina lengo moja tu... Kuwapaka matope viongozi wa chama wa kitaifa na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa lengo la kudhoofisha jitihada za chama kujijenga kwa wananchi na kuendeleza vita dhidi ya ufisadi ambayo imekipatia chama na viongozi wake umaarufu,`` alisema.

Akitoa maelezo ya baadhi ya tuhuma dhidi yake, Mwenyekiti wa Chadema Taifa Bw. Freeman Mbowe, alisema katika uchaguzi wa mwaka 2005 alikikopesha chama Sh. milioni 500 kwa ajili ya kampeni iliyokuwa ikiendeshwa kwa helikopta, na kwamba hata Mbunge wa Moshi Mjini, Bw. Philimon Ndesamburo naye alikikopesha chama zaidi ya Sh. milioni 100.

``Lakini kati ya fedha hizo nimesamehe nusu nzima kwa ajili ya chama na hata zinazoendelea kurejeshwa nusu nusu, zimekuwa zikitumika pia katika kazi za Chama,`` alifafanua.

Akiongea na Nipashe kwa njia ya simu kutoka Dodoma jana, Bw. Wangwe alisema hakubaliani na uamuzi wa kumsimamisha na hivyo atakata rufaa katika Baraza la Chama hicho ambalo ni sawa na NEC ya CCM.

``Jana (juzi) usiku, tulikuwa na kikao cha Kamati Kuu. Mwenyekiti wetu (Mbowe) alisimama na kusema hawezi kuendelea kufanya kazi na mimi. Akasema ama yeye aachie ngazi ama mimi. Nikauliza kwa makosa yepi?

Wakaniambia tu kuwa eti ninakigawa chama. Kwa kweli hawakunisomea kosa lolote," alisema Bw. Wangwe.

Hata hivyo, alisema anajua mambo yanayomponza ni uamuzi wake wa kutaka raslimali za chama ziendeleze ofisi zilizoko wilayani ili chama kipate wanachama wengi zaidi na pili kuifanya CHADEMA iwe na sura ya kitaifa kuliko ilivyo hivi sasa.

Kingine alisema anahisi ni tishio lake kwa uongozi wa juu, hasa baada ya kuonyesha dhamira yake kwamba anataka mabadiliko makubwa ya kiuongozi ili CHADEMA iweze kushika dola kama si kuwa na viti vingi zaidi bungeni.

Kuhusu raslimali, Bw. Wangwe alisema kwamba viongozi wenzake wamekua hawakubaliani naye kwa kutaka ruzuku ya sh. milioni 66 wanayopata kila mwezi, wapeleke kwa kila wilaya angalau laki moja moja tu.

``Mimi nilitaka hizi pesa zitumike kukodia ofisi na kusaidia mambo ya stationery (vifaa vya kuandikia) kwa sababu asilimia 60 za wilaya zote Tanzania hatuna ofisi. Katika hali hiyo unaweza kuwa na ndoto kweli ya kushika dola?`` Alihoji.

Alisema kwamba anaamini CHADEMA haiwezi kupata wanachama wengi zaidi kama haitajenga maofisi kila sehemu na kuongeza wanachama.

``Tunao uwezo wa kupata wanachama lukuki kama tutaacha ubinafsi na kupeleka chama chini zaidi kwa wananchi badala ya kubaki makao makuu. Tuna uwezo wa kushinda urais au tukishindwa basi tukapata wabunge hata 100 na kuwawakilisha vyema wananchi bungeni. Lakini wenzangu, ama kwa sababu wanazozijua wao, ama kwa vile hawana vision wala mission (mtazamo wa mbali na mkakati-kazi) naonekana kikwazo,`` alisema.

Kuhusu kutaka CHADEMA iwe na sura ya kitaifa Bw. Wangwe alisema hilo limekuwa tatizo lingine.

``Ninakupa mfano mdogo tu. Sisi, kutokana na kupata wabunge watano wa kuchaguliwa, tulipata pia nafasi sita za ubunge wa viti maalum.Lakini cha ajabu, nafasi tano zilikwenda mkoa mmoja pekee,`` alisema bila kuutaja na kuongeza kwamba ilitakiwa nafasi hizo zigawanywe kwa kanda.

Alisema anapopigania mambo hayo anaonekana kero kwa wale ambao hawataki mbadiliko kutokana na ubinafsi ama kutokuwa na mtazamo wa mbali.

Alisema hilo la kusimamishwa yeye haliiti mgogoro bali mchakato wa kukisaidia chama.

``Lakini mchakato wetu hapa unaonyesha udhaifu mkubwa wa kiuongozi, tofauti na ule wa Marekani baina ya (Hilary) Clinton na (Barack) Obama ambapo baada ya kutofautiana wamerudi pamoja.

Lakini nadhani nitapigana vita hii na ninaweza kushinda na kuipaisha CHADEMA,`` alisema na kuongeza kwamba atakata rufaa katika kikao cha Baraza.

Alisema, tofauti na gazeti moja lilivyoandika jana, hajawahi kuwa na ugomvi na Mwenyekiti Freeman Mbowe wala Zitto Kabwe.``

Bw. Wangwe pia alionekana kushangazwa na wale wanaompakazia kwamba anatumiwa na CCM.

``Yaani nawashangaa hata wanaokubaliana na hoja kama hizo. Yaani mimi Wangwe niwatumikie CCM ambao nilipigana nao vikali nikawashinda kule Tarime?
Back to top Go down
View user profile
RAIPosts : 10
Join date : 2008-07-07

CHADEMA inapoanza kubomoka na kupoteza umaarufu wake Empty
PostSubject: Re: CHADEMA inapoanza kubomoka na kupoteza umaarufu wake   CHADEMA inapoanza kubomoka na kupoteza umaarufu wake I_icon_minitimeMon Jul 07, 2008 5:22 pm

mtazamo wangu ni huu maana najua muda wa kujisafisha bado upo hivyo wanachotakiwa ni kuzingatia mikakati ya 2010 na wakati wakifikiria hivyo "WASIFANYE" kosa lingine la kumtimua kiongozi yeyote ndani ya chama. Wakitimua kiongozi mwingine that will be a ticket to self distruction indefinitely.
Back to top Go down
View user profile
 
CHADEMA inapoanza kubomoka na kupoteza umaarufu wake
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: Your first category :: POLITIKO (SIASA)-
Jump to: