Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 

 Baada ya CHADEMA kumwaga ugali.....Wangwe amwaga mboga...

Go down 
AuthorMessage
Admin
Admin


Posts : 8
Join date : 2008-06-20

Baada ya CHADEMA kumwaga ugali.....Wangwe amwaga mboga... Empty
PostSubject: Baada ya CHADEMA kumwaga ugali.....Wangwe amwaga mboga...   Baada ya CHADEMA kumwaga ugali.....Wangwe amwaga mboga... I_icon_minitimeThu Jul 03, 2008 8:39 pm

Baada ya CHADEMA kumwaga ugali...Wangwe amwaga mboga

Habari Zinazoshabihiana
CCM yagaragaza tena CHADEMA, NCCR 29.02.2008 [Soma]
Wangwe kuadabishwa na kamati iliyojadili akina Mengi na Malima 10.02.2007 [Soma]
Mbunge amkomalia Spika 09.02.2007 [Soma]

*Alalamikia kuchafuliwa, ubaguzi wa kikabila ndani ya chama
*Awapa viongozi siku 14 kumsafisha, vinginevyo mahakamani
*Akana kutoa siri CCM, adai Mbowe ndiye hukutana nao faragha

Na Mwandishi Wetu

MGOGORO wa uongozi unaorindima ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umeingia katika sura mpya baada ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho aliyesimamishwa hivi karibuni, Bw. Chacha Wangwe, kuwapa siku 14 viongozi wa chama hicho kuthibitisha madai yao kwamba anashirikiana na CCM kukihujumu, vinginevyo atawafikisha mahakamani.

Bw. Wangwe ambaye pia ni Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya chama hicho, aliliambia gazeti hili jana kuwa madai ya viongozi hao yamemchafulia jina na heshima kiasiasa aliyoijenga ndani ya chama hicho kwa gharama kubwa.

Wiki iliyopita katika kikao chake, mjini Dodoma, Kamati Kuu ya CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake, Bw. Freeman Mbowe, ilimsimamisha uongozi Bw. Wangwe kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo kutoa siri za chama hicho kwa viongozi wa CCM.

Bw. Wangwe alituhumiwa pia kukashifu chama hicho, viongozi na watendaji wake, bila kutofautisha kashfa na ukosoaji wa kisiasa na kiutendaji, kwa kutumia wanachama waliochukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama hicho.

Tuhuma zingine ni pamoja na kuwatuhumu viongozi wenzake wa juu na watendaji wake kwa kuwahusisha na ukabila na kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wenye lengo la kukihujumu chama hicho.

Akizungumza katika ofisi za gazeti hili Dar es Salaam jana, Bw. Wangwe alipinga madai hayo na kueleza kuwa hayana msingi na kwamba katika kipindi chote, ameipigania CHADEMA kwa nguvu zake zote na gharama kubwa, bila kuogopa mazingira magumu kwenye harakati hizo.

Alisema akiwa kiongozi wa chama hicho wilayani Tarime, alinyakua jimbo hilo na halmashauri ya wilaya hiyo huku 'wapiganaji' wenzake wakijeruhiwa kwa vipigo, kupata vilema vya maisha, kupoteza ajira na hata maisha.

Kutokana na harakati hizo, waliwezesha kupatikana asilimia 64 ya kura za jimbo hilo ambazo zilichangia ushindi wa CHADEMA na kuiwezesha kupata ruzuku ya sh. milioni 66 kila mwezi na viti maalumu sita bungeni vya chama hicho.

Alisema jitihada zake zilimfanya mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Mbowe kuibuka na kura nyingi kumzidi mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wilayani humo, kwenye uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2005.

Akizungumzia uhusiano wake na Dkt. Amani Kabourou ambaye alikihama chama hicho na kwenda CCM, alisema ni wa siku nyingi hata kabla ya kujiunga na CCM na uhusiano huo haufungamani kwa namna yoyote ile na masuala ya kisiasa kama inavyodaiwa na viongozi wa CHADEMA.

"Dkt. Kabourou nashirikiana naye siku nyingi tangu aliporudi kutoka Marekani, naheshimu uamuzi wake wa kwenda CCM na huo ni uamuzi wake mwenyewe, tangu aende CCM sijakutana naye bali Juni 7 mwaka huu, nilikwenda kwake kuhani msiba wa mama yake mzazi tukiwa na Bibi Maulida Anna Komu," alisema Bw. Wangwe.

Bw. Wangwe alishangaa suala hilo kuhusishwa na hujuma dhidi ya chama hicho na kuzidi kufafanua Katiba ya CHADEMA haina kipengele kinachozuia mwanachama kuwa na uhusiano na wanachama wa vyama vingine, bali tofauti iliyopo ni hoja.

Alimshambulia Mwenyekiti wa Chama hicho, Bw. Mbowe kwa maelezo kuwa amekuwa karibu zaidi na viongozi wengi wa CCM na wakati mwingine wanakutana faragha, lakini kama mwanachama ana uhuru wa kufanya hivyo na hakuna anayempinga kwa hilo.

"Dkt. Slaa (Wilbroad), mkewe ni kada wa CCM aliyekubuhu ni Diwani wa kuchaguliwa wanakaa pamoja, simu, nyaraka zote, wageni wote wanaokuja mama anasikiliza, hawanitendei haki mimi kwa hili," alisema Bw. Wangwe.

Alisema kuengulia kwake ni mkakati ulioandaliwa muda mrefu kumng'oa kwenye nafasi hiyo, kutokana na dhamira yake ya kutaka kufanyika mageuzi ya kweli ndani ya chama hicho.

"Nilisema uongozi uliopo tutaupumzisha, kwani umeshindwa kupeleka chama mbele," alisema Mbunge huyo machachari na kusisitiza kuwa ajenda ya kumsimamisha uongozi haikuwa kwenye mkutano wa Dodoma ila kilichokuwapo ni kuwasilishwa Ripoti ya Tume ya Mzirai, iliyoundwa kuchunguza tuhuma mbalimbali ndani ya chama hicho, lakini suala hilo likaibuliwa.

Alibainisha kuwa tofauti iliyojitokeza kati yake na Bw. Mbowe, ni suala la mgawanyo wa ruzuku kati ya makao makuu kwa upande mmoja na wilaya kwa upande mwingine, jambo alilosema kwa muda mrefu amekuwa akipigia debe chama hicho kujijenga kuanzia chini kwenda juu, jambo linalokinzana na msimamo wa mwenyekiti wake.

"Ninachopigania ni mfumo wa 'bottom up' (kuanzia chini kwenda juu) fedha zipelekwe kwenye vitovu vya mapambano zikajenge chama kwenye maeneo ambayo hakipo, lakini wenzangu wanataka mfumo wa 'up bottom' (juu kwenda chini).

Alisema gharama za kuendesha chama wilayani ni ndogo, kwani endapo kila mwezi zitapelekwa sh. 100,000 zitatosha kulipa pango la ofisi linaloweza kugharimu kati ya sh. 25,000 hadi 30,000 na sh. 70,000 zikabaki kwa matumizi mengine ya ofisi. Mbali na fedha hizo, alishauri pia kutolewa sh. 100,000 nyingine kwa ajili ya kulipa wasimamizi wa ofisi hizo.

"Yeye (Bw. Mbowe) anataka fedha zitumike kwa helikopta, sisemi kwamba helikopta ni kitu kibaya, lakini tuangalie katika mruko tulipata watu wangapi? Lazima tuwe na majimbo, wanachama na matawi ya kutosha, hata kama CCM itatuzidi nguvu, basi angalau tupate majimbo 150, hata ruzuku itapanda.

Alipinga kile alichokiita madeni hewa wanayojilipa viongozi wakuu wa chama hicho kwa madai ya kukikopesha chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ambapo alisema Bw. Mbowe alidai kuikopesha CHADEMA sh. milioni 500, Bw. Philemon Ndesamburo sh. milioni 100 na Bibi Grace Kiwelu sh. milioni 100

"Nilipochaguliwa umakamu niligundua udhaifu huu, mfano kuhitilafiana wakati Baraza Kuu linatoa ratiba ya uchaguzi wa ndani ngazi zote...baadhi uchaguzi hautafanyika kwa sababu hakuna fedha zilizotolewa.

"Tutapataje chama chenye uhai kama hakuna fredha za kuwaewezesha wanachama kugombea? Sheria ya vyama inasema wazi, kuwa Msajili wa Vyama atafuta chama kisipochaguana kwa kuzingatia taratibu zilizopo. Kwa mwendo huu tutazamie mamluki bila uchaguzi," alisema.

Alidai kuwa hadi sasa, Bw. Mbowe ameshajilipa sh. 218,330,543.

Kuhusu ubaguzi wa kikabila, alikariri taarifa ya Tume ya Mzirai iliyobaini kuwa ubaguzi huo upo ikisema katika uongozi wa juu wa chama hicho, wakurugenzi, wenye watu wanane, wanne ni kutoka Kaskazini (Wachagga).


Alisisitiza nia yake ya kupinga kusimamishwa kwa kutumia vikao vya juu vya chama hicho ikiwa ni pamoja na Baraza Kuu, Mkutano Mkuu na hata kulifikisha suala hilo kwa wanachama kama vikao hivyo vitashindwa.
Back to top Go down
View user profile http://viongozitz.friendhood.net
 
Baada ya CHADEMA kumwaga ugali.....Wangwe amwaga mboga...
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: Your first category :: POLITIKO (SIASA)-
Jump to: