Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 
 JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa..

Go down 
AuthorMessage
rekesheiPosts : 17
Join date : 2008-06-20

JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa.. Empty
PostSubject: JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa..   JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa.. I_icon_minitimeSun Jul 13, 2008 9:48 am

Baba mzazi wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana (UVCCM), marehemu Amina Chifupa, jana alikuja juu akisema kwamba majina ya vigogo waliosababisha kifo cha mwanae wataanikwa hadharani tena mbele ya waandishi wa habari hivi karibuni.

Mzee Hamis Chifupa aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba kabla ya mwanae hajafa kuna aliowataja kwa mabaya na mazuri wakiwamo vigogo na wafanyabiashara wazito na kwamba wote watachunguzwa kubaini ni kina nani walihusika.

"Wakati anaumwa alitaja majina ya watu wengi, ili kubaini kama walihusika familia inafanya uchunguzi na baadaye tutatoa majina ya waliohusika hapa hapa," alisema Mzee Chifupa.

Akadai kwamba kutokana na hali hiyo ni dhahiri kwamba mwanae Amina alikufa kabla ya wakati wake kwa vile kuna watu alikuwa akiwataja taja wakati alipokuwa anaumwa.

Hata hivyo alisema uchunguzi kuhusu kifo cha marehemu Amina haufanyiki kama ule wa Tume ambapo watu huitwa na kuhojiwa bali unafanyika kwa kufanyia kazi taarifa za mtoto wao alizosema wakati wa uhai wake. Alipoulizwa wanafamilia ilitaka Amina afariki lini ili iweze kuamini amekufa wakati muafaka alijibu;

"Kufa angekufa lakini sio kwa kipindi hiki kwani wamemuwahisha muda wake ulikuwa bado" Waandishi wa habari walipomuuliza mzee Chifupa kuwa ripoti ya madaktari inaeleza marehemu Amina alikufa kwa ugonjwa gani, alijibu ya kuwa inaonesha kwamba alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na yale ya kiswahili.

Mzee Chifupa alisema mwanae alikuwa mtu wa maajabu na kutolea mfano kimbunga kilichotokea ghafla mara baada ya kuingia ukumbini kwa ajili ya sherehe yake ya kicheni pati.

Waandishi wa habari walipombana mzee huyo kuwa kama anaamini mtoto wake alikuwa mtu wa ajabu ni kwa nini hataki kuamini taarifa zilizoelezwa katika kanisa moja jijini Dar es Salaam kuwa Amina hajafariki bali alichukuliwa msukule na yupo mashamba ya Kibaha alijibu ya kuwa hilo hakubaliani nalo. Hata hivyo alisema milango ipo wazi kwa watu wanaodai wana uwezo wa kumrejesha.

Alisema wakati kifo chake kilipotokea alipokea simu zaidi ya 10 kutoka kwa waganga waliodai wana uwezo wa kumrejesha na aliwataka wafanye hivyo kama wanaweza lakini wameshindwa. Mzee Chipa alisema familia yake inaamini Amina alifariki na yupo peponi.

Kuhusu urithi wake alisema mahakama ilishatoa uamuzi na ilieleza kuwa watu wanaotakiwa kurithi mali zake ni mama yake, baba na mtoto wake.

Hata hivyo hakueleza mali zake alizoacha zina thamani kiasi gani. Kifo cha Amina Chifupa kilichotokea Juni mwaka jana kilifunikwa na utata mwingi kwa sababu kabla ya kifo chake habari zilisema mume wake alikwenda kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana, John Nchimbi akamweleza jambo ambalo lilimuudhi na kuamua kumpa talaka marehemu.

Amina Chifupa alikuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya watumia madawa ya kulevya na wakati fulani aliwahi kutamka kwamba ana majina yao na alikuwa tayari kutaja majina yao.
Back to top Go down
View user profile
dRUPosts : 5
Join date : 2008-07-15

JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa.. Empty
PostSubject: Re: JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa..   JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa.. I_icon_minitimeWed Jul 16, 2008 1:12 am

Mungu amuweke pahala pema peponi marehemu. Hakuna mtu yeyote ambaye hukubali kirahisi kukabiliana na hali ya kupotelewa na mpendwa yeyote ndani ya familia. Yote ni kazi ya mungu na si vyema sisi kama waja wake kutaka ama kuwa washindani kwa mara kuhisi hili ama lile kati yetu na kumbe mola mwenyewe ndiye aliyekuwa muamuzi wa yote tunayoyajiri hapa duniani.

Ninasema yote haya nikiwa na lengo la kutaka familia na wote ambao tuliguswa na kifo cha Amina kuamini kwamba yote hayo na matakwa ya mola hivyo si vyema wakati kama huu kuanza tena mjadala kama huu maana hauna faida yeyote si kesi ya kwenda mahakamani kumtafuta mkosefu na wala si jambo ambalo litapata ufumbuzi wa marehemu kurudi tena duniani.

Tumrejee mungu na kumuombea marehemu nafuu ya adhabu ya kaburi na siyo tena kuingia kutajana majina (isaidie nini???).
Back to top Go down
View user profile
pedejeePosts : 9
Join date : 2008-07-02

JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa.. Empty
PostSubject: Re: JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa..   JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa.. I_icon_minitimeWed Jul 16, 2008 8:34 am

dRU wrote:
Mungu amuweke pahala pema peponi marehemu. Hakuna mtu yeyote ambaye hukubali kirahisi kukabiliana na hali ya kupotelewa na mpendwa yeyote ndani ya familia. Yote ni kazi ya mungu na si vyema sisi kama waja wake kutaka ama kuwa washindani kwa mara kuhisi hili ama lile kati yetu na kumbe mola mwenyewe ndiye aliyekuwa muamuzi wa yote tunayoyajiri hapa duniani.

Ninasema yote haya nikiwa na lengo la kutaka familia na wote ambao tuliguswa na kifo cha Amina kuamini kwamba yote hayo na matakwa ya mola hivyo si vyema wakati kama huu kuanza tena mjadala kama huu maana hauna faida yeyote si kesi ya kwenda mahakamani kumtafuta mkosefu na wala si jambo ambalo litapata ufumbuzi wa marehemu kurudi tena duniani.

Tumrejee mungu na kumuombea marehemu nafuu ya adhabu ya kaburi na siyo tena kuingia kutajana majina (isaidie nini???).

dRU tatizo nadhani hapa ni imani zetu watanzania kiujumla maana ukiangalia aliyosema mzee chifupa on the basis of faith, nadhani hajaonyesha nini nia yake hasa zaidi. Maana kuna kipindi alisema kwamba marehemu amina chifupa alifariki kwa ugonjwa wa kisukari sijui na nini tena *hiyo ilikuwa ripoti ya daktari aliyopewa* ambayo aliitaja hivi karibuni baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari, now lets go back to few days after amina's death, alisema kwamba ni kazi ya Mungu na wengi tukamuelewa, but then tokea kipindi hicho akaanza kusema kwamba ushirikina, mara sijui ameuliwa kitu ambacho kinakuwa kigumu kwa wengine kuelewa ni nini hasa mzee Chifupa anachojaribu kutuletea kwenye jamii.
Back to top Go down
View user profile
Sponsored content
JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa.. Empty
PostSubject: Re: JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa..   JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa.. I_icon_minitime

Back to top Go down
 
JUST IN: Mzee Chifupa adai kwamba waliohusika na kifo cha Amina kutajwa..
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: Your first category :: POLITIKO (SIASA)-
Jump to: