Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 

 CCM Ina nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi mkuu 2010

Go down 
AuthorMessage
rekesheiPosts : 17
Join date : 2008-06-20

CCM Ina nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi mkuu 2010 Empty
PostSubject: CCM Ina nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi mkuu 2010   CCM Ina nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi mkuu 2010 I_icon_minitimeTue Jul 15, 2008 10:10 am

Najua wengi wanaweza kushangaa kwa nini kichwa cha habari kipo kama hivyo kilivyo na wengine hata kunifikiria vibaya kwa nini nimeandika hivyo. Lakini ukweli ni kwamba siku zote katika masuala ya siasa, uvumilivu na uwezo wa kuwa na mbinu mbali mbali ndio mambo makuu mawili ambayo huchangia katika chama chochote kile kuendelea kukaa madarakani. Baada ya kusema hayo ni dhahiri kwamba hadi hivi sasa tukawa tunaelekea kuwa pamoja katika kuelewa kwa nini nimesema ccm ina nafasi kubwa kushinda 2010.

Ukweli ni kwamba NDIO NI KWELI KUNA MAKUNDI NDANI YA CCM ambayo kwa sasa huonyesha kama kuna mpasuko mkubwa ndani ya chama, na hata wale wachambuzi wa siasa "baadhi yao" wanaona hilo ni kama jambo la kusambaratisha chama hivyo kukifanya chama kionekane dhaifu. Swali la kujiuliza, je haya makundi yalianza leo ? Jibu la haraka haraka ni hapana. Makundi hutokea muda wowote ule, aidha katika siasa, dini, familia na hata katika mkusanyiko wa watu. Ichukulie kukatokea makundi ndani ya familia moja (hapa tuseme ccm). Hayo makundi hupigania kwa sababu moja kuu ambayo ni maslahi ya chama chao na SI CHAMA KINGINE. Sasa unapokuja katika chaguzi kuu ambapo mkusanyiko wa vyama vya siasa vingi hujumuishwa, wengi huenda na kudhania ya kwamba kwa kuwa familia moja (ccm) ina mpasuko/makundi basi ndio wakati muafaka wa kukipasua chama hicho na kukisambaratisha, na wengi hukimbilia huo mkumbo na kufikiria hivyo. Lakini ukweli ni kwamba hata kama makundi yawe mengi kiasi gani, maslahi ya chama ndio huwa namba moja.
Sina uhakika vyama vya siasa vina mikakati gani ya kushinda katika uchaguzi mkuu 2010, na kama wanategemea huo mpasuko/makundi ndani ya ccm kama strategy yao kushinda, basi ukweli ni kwamba naweza kusema UCHAGUZI 2010 WAPINZANI WAMESHINDWA. Tuchukulie mfano wa makundi yaliyojitokeza mwaka 2004 ambapo kulikuwa na kundi la Jakaya Kikwete, John Malecela, Prof. Mark Mwandosya, Magufuli,Sumaye na wengine (walikuwa wagombea 11 toka ccm). Na mpambano huo wa kugombea kukiwakilisha chama cha mapinduzi CCM ulikuwa mkali zaidi kati ya Kikwete na Malecela, lakini pindi ilipobainika tu kwamba Kikwete ndiye mwakilishi wa chama chake katika uchaguzi mkuu nafasi ya urais, basi Malecela alimuunga mkono Kikwete papo hapo na kuanza mikakati ya kufanya kampeni ya kitaifa.
Sasa swali kwa viongozi na wenyeviti taifa wa vyama vya upinzani, je mpo tayari (kifedha, mikakati, mbinu n.k) kuishinda ccm katika uchaguzi mkuu 2010 ? Exclamation
Back to top Go down
View user profile
 
CCM Ina nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi mkuu 2010
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: Your first category :: POLITIKO (SIASA)-
Jump to: