Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 

 Kisa cha mzee wa kichaga

Go down 
AuthorMessage
RAIPosts : 10
Join date : 2008-07-07

Kisa cha mzee wa kichaga Empty
PostSubject: Kisa cha mzee wa kichaga   Kisa cha mzee wa kichaga I_icon_minitimeThu Jul 17, 2008 7:28 pm

Mzee mmoja wa kichagga tajiri kwa jina la MDAWA alipata ajali mbaya sana ya gari. Alipoteza fahamu na kupelekwa KCMC huku matumaini ya kupona yakiwa yametoweka kabisa. Kutokana na juhudi za madaktari (pengine na Mungu wake) aliweza kupata fahamu baada ya wiki tatu.Muda wote huo familia yake ilikuwa ikokaribu naye kusubiri
litakalotokea. Mkewe na Watoto wake watatu waliruhusiwa kuwa naye pale ICU (Intensive Care Unit) kwa zamu. Basi baada ya kupata fahamu nesi aliyekuwa anamhudumia alimwambia;

NESI: Baba pole sana

MZEE MDAWA: Unanipa pole kwani nini kimetokea?

NESI: Baba ulipata ajali mbaya sana ya gari wiki tatu zilizopita.

MZEE MDAWA: Kweli, Kari yangu itakuwa imepona?

NESI: Hapana imeharibika kabisa Baba.

MZEE MDAWA: Hai jamani FII EKIS (VX) yangu. Niliinunua kwa bei kubwa mno. Sasa nitapata wapi nyingine...aaaiiii aaaaaaiii aaaaaiiii!

NESI: Baba usilie, hilo mbona ni kidogo? Unajua mkono wako wa kushoto umekatika kabisa?

MZEE MDAWA: Mkono wa kushoto? Umekatika? Ule mkono niliovaa ile saa yangu ya bei mbaya? Yaani saa yangu nayo imekwenda? Aaaiiii....aiiii...aiiiii, jamani saa yangu.

NESI: Baba acha kulia, utaumia zaidi

MZEE MDAWA: Hapana mwanangu, kama kari yangu na saa fyote fimekwenda kwa nini roho isiniume? Hifyo fitu ni fya bei mbaya sana ati...

NESI: Baba tulia, familia yako iko hapa wanataka kukupa pole.

MZEE MDAWA: Iko hapa ee? Mama Sikola, uko hapa?

MAMA: Ndiyo ! mume wangu, siwesi kukuacha mwenyewe. Pole sana mpenzi. Tunamshukuru Mungu sasa unaongea. Yesu asifiwe sana !

MZEE MDAWA: Sawa, Kodilafu uko hapa?

GODLOVE: Ndiyo Mzee, siwezi kukuacha mwenyewe katika hali hii. Pole sana baba.MZEE: Sikola, na wewe uko hapa?

SKOLA: Ndiyo Baba, hatuthubutu kukaa mbali na wewe ukiwa katika hali hii baba. Ni hali ya kutisha sana .

MZEE: Na huyu kitinda mimba wangu Ferenaisi, yuko hapa?

Verynice: Niko hapa baba, nyumba yote iko hapa kukupa pole.

MZEE: Basi nyie wote hamna akili hata mmoja. Yaani Mmekuja wote hapa, dukani kabaki nani leo? Yaani munanona kari yangu ni hiyo imepika msinga tayari na saa yangu ya bei
mbaya imepotea badala ya kukaa dukani wote munaongosana kuja huku KCMC. Nyie ni wajinga wa mwisho kabisa.
Back to top Go down
View user profile
 
Kisa cha mzee wa kichaga
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: UDAKU,UMBEA, FIKSI, NYEPESI NYEPESI-
Jump to: