Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 

 BREAKING NOW: Sababu ya kuvamiwa MWANAHALISI yagundulika

Go down 
AuthorMessage
RAIPosts : 10
Join date : 2008-07-07

BREAKING NOW: Sababu ya kuvamiwa MWANAHALISI yagundulika Empty
PostSubject: BREAKING NOW: Sababu ya kuvamiwa MWANAHALISI yagundulika   BREAKING NOW: Sababu ya kuvamiwa MWANAHALISI yagundulika I_icon_minitimeSat Jul 19, 2008 8:00 pm

JESHI la Polisi nchini linaendelea kumchunguza Mhariri wa Gazeti la Mwana Halisi Bw. Saed Kubenea kwa tuhuma za kuhusika kusambaza akaunti za baadhi ya wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwenye mtandao wa Internant kinyume na sheria.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Bw. Robert Manumba, baada ya makachero wa Jeshi la Polisi kuvamia na kuipekua ofisi ya gazeti hilo na nyumbani kwa Bw. Kubenea na baadaye kuchukua kompyuta kwaajili ya kufanya uchunguzi zaidi.

Alisema Bw. Kubenea na mfanyakazi mmoja wa NBC, Bw. Peter Msaki, wamehusishwa na tuhuma za kuchukua akaunti za watu kwa siri na kisha kuzisambaza katika mtandao.

Kwa mujibu wa Bw. Manumba, Polisi ilipata malalamiko kutoka kwa uongozi wa benki hiyo kuwa baadhi ya akaunti za wateja wake zimekuwa zikisambazwa katika mtandao bila ya wao kuwa na taarifa na kuomba wahusika wachunguzwe.

"Baada ya kupata taarifa za awali, tuliamua kuwahoji watuhumiwa ambao ni Bw. Kubenea na Bw. Msaki na kabla ya kwenda kufanya upekuzi ofisini kwa Bw. Kubenea na nyumbani kwake, tulifuata taratibu zote za kisheria," alisema Bw. Manumba.

Alisema kuna taratibu za kisheria zinazopaswa kufuatwa kabla ya kufanya uchunguzi kwenye akaunti ya mtu ili mwisho wa siku sheria ionekane imefutawa.

Hata hivyo alisema kuwa hizo ni tuhuma na uchunguzi unaendelea na kuongeza kuwa baada ya kuwahoji waliachiwa huru ili waweze kuendelea na shughuli zao lakini watakapohitajika watatakiwa kuja kuisaidia Polisi.

Alisisitiza kuwa hata Polisi inaweza kuchunguza akaunti ya mtu kwa kufuata sheria na taraibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kuomba kibali kutoka mahakamani kama ina mashaka.

Alisema pia uongozi wa benki husika unapaswa kuwa na taarifa na kazi inayochunguzwa inabaki kuwa siri.

Hata hivyo Bw. Manumba alipoulizwa ni wateja gani wa benki hiyo ambao wamelalamika akaunti zao kuwekwa katika mtandao hakuweza kuwataja kwa madai kuwa ni siri kwa sasa.

"Kutaja majina ya ambao akaunti zao zimewekwa kwenye mtandao kwa sasa ni mapema mno, tuache uchunguzi uendelee kwanza," alisisitiza.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi limesisitiza wananchi kuwa makini na baadhi ya watu wanaojihusisha na mambo ya utapeli wa kutumia simu za mkononi na katika mtandao wa kompyuta.

Alisema baadhi ya matapeli hao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi, wafanyabiashara na watu maarufu kuchukua fedha za watu.

Alisema wananchi wanatakiwa kutoa taarifa Polisi pindi wanapoona kuna mtu anataka fedha wakati hamjui na wala hausiki na kampuni yoyote ya mtandao wa simu.
Back to top Go down
View user profile
 
BREAKING NOW: Sababu ya kuvamiwa MWANAHALISI yagundulika
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: Your first category :: POLITIKO (SIASA)-
Jump to: