Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 

 bajeti ya serikali yapondwa na.........

Go down 
AuthorMessage
rekesheiPosts : 17
Join date : 2008-06-20

bajeti ya serikali yapondwa na......... Empty
PostSubject: bajeti ya serikali yapondwa na.........   bajeti ya serikali yapondwa na......... I_icon_minitimeFri Jun 20, 2008 5:48 pm

Wasomi Chuo Kikuu waiponda bajeti wadai imekosa vipaumbele
Na Kizitto Noya

WACHUMI na wanataaluma wa Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu chaDar es salaam (UDSM) wameponda kima cha chini cha mshahara wa Sh100,000 kwa maelezo kuwa kitaongeza mfumuko wa bei na kuchochea rushwa katika jamii.


Wakizungumza juzi kwenye Mdahalo wa bajeti ya mwaka 2008/2009 uliofanuika katika UDSM walisema pia kuwa, wameshindwa kutabiri utekelezaji wa bajeti hii kwa kuwa hakuna kanuni ya kitalaamu iliyotumika kupanga vipaumbele vyake.


Profesa Sam Maghimbi wa Idara Sayansi ya Jamii UDSM alisema kwa viwango vyovyote vile vya maisha, kima cha chini cha Sh100,000 na hata kile cha Juu cha Sh720,000 kwa mwezi, havimwezeshi Mtanzania kumudu gharama za maisha kwa sasa.


Alisema Sh100,000 ni ndogo na haimwezeshi mtu kuondokana na umaskini kwa njia rahisi ya mikopo kwenye taasisi za fedha.


''Mshahara sio zawadi, ni haki ya kila anayefanya kazi. huwezi ukaongelea maendeleo wakati umesahau walalahoi. Mishahara ya watumishi ni midogo na serikali inajua hilo ndio maana imekubali kuacha kuwakata kodi,'' alisema.


Alisema kiasi hicho cha fedha kitaipunguzia serikali mapato kwa kuwa haitakitoza kodi na kitachochea rushwa kwa watumishi wa taasisi za umma.


Naye Profesa Delpin Rwegasira alisema bajeti ya mwaka huu haina tija kwa wajasiriamali wadogo na itaongeza mfumuko wa bei kwa kuwa imeongeza kodi bila kuwa na mikakati ya uzalishaji.


''Gharama za vyakula katika nchi maskini ni kubwa kuliko hata nchi tajiri na kibaya zaidi hatuna hakika kodi hiyo iliyoongezwa itakusanywaje wakati hakuna mikakati ya uzalishaji,'' alisema.


Profesa Maurice Mbago alisema ingawa muundo wa bajeti za serikali zinatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine, kanuni za maandalizi yake zinafanana, lakini hana hakika endapo Wizara ya Fedha na Uchumi ilitumia kanuni hizo katika kuiandaa bajeti hiyo.


Alitaja kanuni hizo kuwa ni uwazi, uwezo wa kutabiri mwelekeo wa uchumi, uchambuzi wa kina, ushirikishwaji wa wadau, uhalisia na kupangwa kulingana na mapato.


Alisema bajeti hii haikuweza kutabiri kasi ya mfumko wa bei na matokeo yake imeweka mabadiliko yasiiyokuwa na tija wala uwiano wa kipato na kasi ya kumfuko wa bei hiyo.


Profesa Nehemiah Osoro alitaja kasoro nyingine katika bajeti hiyo kuwa ni kodi wanayotozwa wafanyakazi (PAYE) kutotozwa kulingana na kanuni ya kulipa kadiri unavyopata.


Alisema kodi ya PAYE ya mwaka huu, haitumii kanuni hiyo badala yake imeweka tofauti inayolingana kwa makato jambo ambalo ni tatizo kwa wafanyakazi.


''Naye Dk Adolf Mkenda alisema namna pekee ambayo serikali inaweza kufanikiwa katika kutekeleza bajeti yake ni kutafuta vyanzo mbadala vya mafuta badala ya kutegemea petroli na dizeli ambayo hata kama haikuongezwa kodi, bei yake bado iko juu katika soko la dunia.''
Back to top Go down
View user profile
 
bajeti ya serikali yapondwa na.........
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: Your first category :: POLITIKO (SIASA)-
Jump to: