Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 

 Hatari ya kuzaliwa mtoto wa kike Tanzania

Go down 
AuthorMessage
RAIPosts : 10
Join date : 2008-07-07

Hatari ya kuzaliwa mtoto wa kike Tanzania Empty
PostSubject: Hatari ya kuzaliwa mtoto wa kike Tanzania   Hatari ya kuzaliwa mtoto wa kike Tanzania I_icon_minitimeSat Jul 19, 2008 8:03 pm

SHUHUDA zinazotolewa na watu mbalimbali zinaonesha kuwa mtoto wa kike anaandamwa na ukatili mwingi kuliko wa kiume. Kwa jamii za Kiafrika, jambo hilo linaonekana kutokuwa na ubishi.

Mara nyingi ukatili unaowaandama ni kwa sababu tu ya kuzaliwa wasichana na si kwamba wazazi wana-chuki nao.

Mfano wapo wazazi wanaomtazama mtoto wa kike kama kitega uchumi cha hapo baadaye.

Wazazi wa aina hiyo ambao wako wengi katika maeneo ya wafugaji, wamekuwa wakimpigia 'mahesabu' mtoto wa kike hata kabla ya kuvunja ungo au kuandikishwa darasa la kwanza.

Wazazi wa aina hiyo mara nyingi hukosa mipango ya kuwaendeleza wasichana kielimu na kwao imekuwa jambo la kawaida kuwasikia wakijisifu kuwa na mali kubwa nyumbani kwao, na wakiulizwa aina ya mali wanayojisifu, watajibu ni mtoto wa kike.

Imefika hatua ambapo wazazi wenye mtazamo wa aina hiyo hushangilia sana mara tu anapozaliwa mtoto wa kike ndani ya familia zao kutokana na dhana waliyojenga kuwa mtoto wa kike ni sawa na kitega uchumi.

Wengine wamefikia hatua ya kuchukua mahari ya kuwaozesha watoto wao wakiwa kwenye vilabu vya pombe.

Tabia hii inawanyima haki watoto wa kike ambao wana haki sawa na wale wa kiume. Kibaya zaidi hata hawapewi nafasi ya kutoa maoni yao.

Baadhi ya watoto wamekuwa wakilazimishwa kuolewa wakiwa na umri ni chini ya miaka 18 wakati mwingine na wazee wanaolingana na wazazi wao.

Wengi wao huingia katika taasisi hiyo ya ndoa bila kujua hata majukumu yao kama wana ndoa na hivyo kujikuta wakifanyiwa ukatili tena wa kijinsia.

Wanachoambulia ni maumivu ya mwili na akili hadi inafikia hatua ya kuchukia maisha ya ndoa na kuamua kukimbia na kwenda kuishi mitaani.

Wengine wanaishia kuambulia vipigo kutoka kwa wanaume waliowaoa ambao hawana hata chembe ya utu ambao hudhani njia pekee ya kumuelimisha mtu ni kwa kutoa vipigo.

Katika maeneo ya wafugaji watu wenye umri mkubwa mara nyingi ndio wanaopenda kuoa wasichana wenye umri mdogo kwa kisingizio kuwa wanataka 'wanyooshwe mgongo.'

Yupo mtoto ambaye aliolewa akiwa na umri mdogo wa miaka 16 ambaye aliwahi kupigwa na kuunguzwa sehemu za siri na mumewe akimtuhumu kuwa anafanya mapenzi na vijana wenzake.

Baadaye iligundulika kuwa licha ya kulazimishwa na mume wake ambaye ni mzee pia mtoto huyo alikuwa amefanyiwa unyanyasaji mwingine wa tohara.

Makabila yanayoendeleza mila hiyo yanafanya hivyo ili kuwapunguzia wanawake tamaa ya wanaume na wale waliopo katika ndoa wasiweze kutoka 'nje'.

Kutokana na vipigo wanavyopata watoto wanao ozeshwa katika umri mdogo, wengi wao wamefikia hatua wanaamini kuwa wanaume ni watu hatari ndani ya jamii.

Wengine wameota sugu kutokana na vipigo hadi imefika hatua kwenda kufanya ukahaba mitaani. Uzoefu unaonesha kuwa mara nyingi ndoa za utotoni zinakuwa ni mapito ya kuelekea kwenye ukahaba.

Katika hali hiyo ya kuuza mwili wakidai wanatafuta maisha, kumbe wanahatarisha maisha yao na kujiweka katika hatari ya kuambukizwa virusi vinavyosababisha UKIMWI (VVU).

Wakishajihusisha na ukahaba, inakuwa vigumu kubadili tabia. Mbali na hiyo wapo watoto wa kike walioozeshwa katika umri mdogo ambao wamekumbana na vitisho vingi ikiwa ni pamoja na kutishiwa kuuawa na waume zao.

Watoto wengine walioolewa katika umri mdogo waliojaribu kukimbia vipigo, wamejikuta wakikumbana na vitendo vya kikatili ikiwa ni pamoja na kubakwa wakiwa mikoni mwa polisi.

Matukio ya aina hii yameripotiwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari hapa nchini.

Mfano yupo mtoto mwingine wa miaka 16 anayedaiwa kulazimishwa na wazazi wake kuolewa, lakini alikataa na kuamua kukimbilia kwa mjomba wake.

Alipoulizwa alisema alikuwa akipinga uamuzi huo kwakuwa hakushirikishwa. Kimsingi hoja ya mtoto huyo ilikuwa na mantiki kubwa lakini hakupewa nafasi ya kusikilizwa.

Hata hivyo mjomba wake hawakuwa tayari kumpokea kwa madai kwamba wazazi wameishapokea mahari na hivyo hawawezi kukaa na mke wa mtu.

Mtoto huyo alilazimika kwenda kwa shangazi yake ambako nako hakupata msaada. Alipoenda Polisi aliambiwa kwa umri aliokuwa nao ni sahihi kuolewa.

Mtoto huyo aliamua kwenda kuolewa na mzee huyo. Kibaya zaidi mzee huyo tayari alikuwa amefiwa na mke wake lakini hakuna aliyejua kiini cha kifo chake. Baadaye iligundulika kuwa mke wa mzee huyo alikufa kwa UKIMWI.

Nyuma ya mtoto huyo wapo wengi wanaokumbana na matatizo ya aina hiyo lakini wanashindwa kulindwa na mfumo mzima wa jamii. Kimsingi ili watoto hao waweze kupata ulinzi ni lazima jamii iweke mkakati madhubuti wa kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Polisi nao wapewe elimu na sio kujiwekea mipaka ya kazi yao wakati watoto wadogo wakiendelea kuvunjiwa haki zao.

Mtoto wa kike ana haki ndani ya familia na ana wajibu wa kulindwa dhidi ya vitendo vya kikatili. Kumlazimisha mtoto mwenye umri mdogo kuolewa ni kuhatarisha maisha yake.
Back to top Go down
View user profile
 
Hatari ya kuzaliwa mtoto wa kike Tanzania
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: HALI HALISI YA MAISHA-
Jump to: