Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 

 BUNGE HOI.

Go down 
AuthorMessage
rekesheiPosts : 17
Join date : 2008-06-20

BUNGE HOI. Empty
PostSubject: BUNGE HOI.   BUNGE HOI. I_icon_minitimeFri Jun 20, 2008 5:50 pm

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea kuwa moto kiasi cha kumfanya Waziri wa Fedha na Mambo ya Uchumi, Mheshimiwa Mustafa Mkulo, leo kukabiliwa na kazi ya ziada katika kupangua hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wabunge wakati wa kuhitimisha mjadala wa hotuba yake ya bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2008 na 2009.

Leo, Mheshimiwa Mkulo anatarajiwa kutoa majibu ya hoja zote, zikiwemo zile zinazofuatiliwa na Watanzania wengi zaidi ambazo ni juu ya soo la urejeshwaji wa fedha kiasi cha Sh. Bilioni 216 zilizoko mikononi mwa watu wachache waliozikopa kupitia mfuko wa kuuza bidhaa nje, CIS, mapesa yaliyochotwa Benki Kuu, BoT kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje, EPA na taarifa juu ya ujenzi wa majengo pacha ya BoT, yanayodaiwa kugharimu zaidi ya Sh. Bilioni 500 za walipa kodi.

Aidha, maelezo kuhusu namna Serikali itakavyohakikisha kuwa hali ya maisha magumu kwa Watanzania inapunguzwa makali inatarajiwa pia kutolewa ufafanuzi na Waziri Mkulo wakati wa majumuisho yake ya leo, sambamba na malalamiko juu ya kiwango kidogo cha mishahara kinacholipwa kwa wafanyakazi wa kima cha chini.

Wakati wa kuchangia hotuba hiyo ya bajeti iliyosomwa na Waziri Mkulo Alhamisi ya wiki iliyopita, wabunge kadhaa waliibana Serikali na kutaka maelezo juu ya mambo hayo na mengine mbalimbali, hasa yahusianayo pia na uimarishaji wa sekta ya kilimo.

Akitoa mchango wake jana, Mbunge wa Same Mashariki , Mheshimiwa Anne Kilango (CCM), alimtaka Waziri Mkulo afafanue kwa undani juu ya mapesa ya CIS yaliyokopwa tangu mwaka 1992 na kisha wahusika wake kutozirejesha Serikalini.

\"Unaweza kudanganya watu wachache wakati wote, lakini huwezi kudanganya watu wote kwa wakati wote,\" akasema Mhe. Kilango wakati akijenga hoja zake za kuibana Serikali, jana.

Aidha, kama ilivyokuwa kwa wabunge wengine, Mhe. Kilango pia alimpa Waziri Mkulo jukumu la kuelezea hatua iliyofikiwa katika urejeshaji wa mapesa yaliyochotwa EPA.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Mhe. Fred Mpendazoe (CCM) amemtaka Waziri Mkulo kutaja bila kificho majina ya wote waliorudisha fedha za EPA.

Aidha, Mhe. Mpendazoe akaiasa Serikali kuwa kamwe isijaribu kuligeuza suala hilo kuwa ni la siri, kwani lina umuhimu mkubwa kwa taifa.

Pia Mhe. Mpendazoe akaitaka Serikali kueleza hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Kamati Teule ya Bunge, ambayo ilifuatilia suala la mkataba tata baina ya Serikali (kupitia TANESCO) na kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond.

Miongoni mwa wabunge waliomtaka Waziri Mkulo aeleze kuhusu mshahara ni Mbunge wa Karagwe, Mhe. Gosbert Blandes (CCM).

Kwa nyakati tofauti, wabunge wa upinzani nao walimbana mara kadhaa Waziri Mkulo juu ya bajeti aliyosoma, hasa kupitia hotuba ya bajeti yao mbadala iliyosomwa na Kiongozi wa Kambi yao, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (CUF), ambaye alitaka maelezo ya kina kuhusu mapesa yaliyotumika katika ujenzi wa majengo pacha ya Benki Kuu nchini, BOT na pia suala la EPA.

Kama kawaida yake, mbunge wa Jimbo la Karatu, Mhe. Dk. Wilbroad Slaa (CHADEMA), aliposimama kidete na kumtaka Mkulo asiache kuelezea suala la EPA na mengineyo yenye maslahi kwa wananchi, kama ilivyokuwa kwa Mhe. Suzan Lymo wa Viti Maalum (CHADEMA).

``Inatia moyo kwamba Bunge la sasa limekuwa moto juu... zile enzi za wabunge wa CCM kuonekana kama ni watu wa kukubali kila kitu zinaelekea kwisha na hivyo kuleta matumaini ya maisha bora kwa Watanzania,`` amesema Mbunge mmoja wa kambi ya upinzani.

Mkulo anatarajiwa kutoa majibu ya hoja mbalimbali za Wabunge, mara baada ya wabunge wanne waliosalia kumaliza kutoa michango yao asubuhi ya leo.
Back to top Go down
View user profile
 
BUNGE HOI.
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: Your first category :: BUNGE LA TANZANIA(DODOMA)-
Jump to: