Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 

 Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ?

Go down 
AuthorMessage
rekesheiPosts : 17
Join date : 2008-06-20

Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? Empty
PostSubject: Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ?   Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? I_icon_minitimeSat Jun 21, 2008 8:42 pm

Asalaam Aleykum, karibuni tena siku ya leo katika baraza la maongezi ya watanzania popote pale walipo. Leo nimeamua kuandika habari hii yenye kuonyesha maswali mawili matatu ambayo kwa kweli nisingependa niyajibu mimi binafsi bali nitawaachia wasomaji waweze kuhumu wenyewe.

Hivi karibuni, bila shaka utakuwa umesikia habari za mbunge Anna Kilango (mke wa mzee Malecela) akitoa hoja zake bungeni. Namshukuru kwa kuonyesha ujasiri wa aina yake. Baadhi ya maneno aliyokuwa akiyatamka ni kama yafuatayo, "Baadhi wanalisema kwa madoido huku wengine tukilisema kwa upole lakini wote hatuogopi wala kutishwa ndani ya Bunge,`` LAKINI kabla ya hapo alisema haya, "hakuna mbunge anayeogopa kuzungumzia suala la ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu (EPA) na kwamba halipaswi kuwagawa wabunge". Kwa kweli haya ni maneno ya kijasiri kwa kiongozi yeyote yule aliyepo bungeni.

Lakini cha kushangaza ni kwamba, inakuwaje mbunge huyu huwa anaanza kunyoosha mdomo wake pale baada ya waheshimiwa wabunge wengine wakishaanza kutoa hoja? Sisemi kwamba anachofanya ni kibaya, la hasha, lakini ukweli ni kwamba yeye alikuwa bungeni muda kidogo sasa, ina maana mambo haya ya EPA anayajua leo? Alikuwa wapi kipindi chote hicho ?....Hivi karibuni mbunge huyu amekuwa akisikika mara kwa mara na wengine wakidai kwamba anatafuta nafasi ya juu ya uongozi, mfano uwaziri ili apate ulaji, wengine wakidai kwamba anatafuta umaarufu tu. Hayo ndio baadhi ya maoni ya waliokuwa wakisikika wakiongea.

Kama ni kweli mama Kilango ana nia ya kutetea maslahi ya wananchi, je yupo huru kurudi hadi katika nyakati zileeee ambazo mume wake alikuwa waziri mkuu ?
Baadhi ya wapambe wake hivi karibuni wamekuwa wakimtetea bila ya sababu za msingi na kumpanda ukidhani malaika, lakini ukweli ni kwamba UKWELI SIKU ZOTE HAUJIFICHI, kumaanisha kwamba kama kweli ana nia njema basi hiyo nia itaonekana na kama ndio ameficha makucha yake basi nayo pia yataonekana.

Haya ni machache kabisa, ila ningependa kwa leo kuishia hapa, na nitaongezea machache hapo baadae.


[img][/img]
Back to top Go down
View user profile
pedejeePosts : 9
Join date : 2008-07-02

Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? Empty
PostSubject: Re: Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ?   Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? I_icon_minitimeWed Jul 02, 2008 1:40 pm

tatizo hapa ni kwamba hawa viongozi sio kwamba hawana nia nzuri, no, wanazo sana isipokuwa wengi wao wametanguliza matumbo yao makubwa mbele. huwezi kukuta viongozi waadirifu hata siku moja wakati ukitazama vizuri kwa ukaribu wengi wanatetea maslahi binafsi.
asante
Back to top Go down
View user profile
rekesheiPosts : 17
Join date : 2008-06-20

Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? Empty
PostSubject: Re: Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ?   Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? I_icon_minitimeWed Jul 02, 2008 2:58 pm

kwa watu wanaomjua anna kilango tulijua kwamba hizo kelele sio ngeni kwetu na wala sio mwisho wa yeye kutoa maneno kama yale ili kupata exposure ya muda mfupi.
Back to top Go down
View user profile
RAIPosts : 10
Join date : 2008-07-07

Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? Empty
PostSubject: Re: Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ?   Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? I_icon_minitimeMon Jul 07, 2008 5:19 pm

huyu mama kwisha kabisa
Back to top Go down
View user profile
RAIPosts : 10
Join date : 2008-07-07

Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? Empty
PostSubject: Re: Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ?   Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? I_icon_minitimeThu Jul 17, 2008 8:37 am

LADIES AND GENTLEMEN, HERE SHE GOES AGAIN. AS THEY SAY IT, THE SAGA CONTINUES.

Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Bi. Anna Kilango Malecela, amesema mkakati alionao sasa ni kuendelea kukemea baadhi ya viongozi na watu wachache wanaoonyesha mwelekeo wa kuendelea kumiliki na kuhodhi mapato ya nchi kwa maslahi yao binafsi.

Aliyasema hayo jimboni kwake jana wakati akizungumza na wanahabari katika mahojiano maalum.

``Ni vyema niwaelimishe wananchi kikamilifu kwamba, wabunge wote wanaoendelea kuchachamaa bungeni au majukwaani wanachokitafuta ni kikubwa zaidi kuliko kupambana na mafisadi,`` alisema.

Aliongeza kuwa, uamuzi huo unatokana na ukweli kwamba wapo baadhi ya viongozi wachache pamoja na kikundi kidogo kinachoendelea kuhodhi mapato ya nchi isivyo halali.

Alisema kwa kipindi kifupi, baadhi ya viongozi ndani ya serikali wameonekana kutoridhika na kipato wanachokipata na badala yake wametumia mianya ya madaraka waliyonayo kumiliki fedha na rasilimali za nchi isivyo halali.

``Endapo kwa umoja wetu kama wabunge ndani ya Bunge hatutapambana na hali hii, hatua ya watu wachache wenye uchu na fedha za walalahoi kutalipeleka taifa mahala pabaya`` alionya.

Aliitaka jamii kutambua kuwa wabunge wote wanaochachamaa bungeni au majukwaani wanachokitaka ni kikubwa zaidi kuliko kupambana na mafisadi.

Alisema kinachopiganiwa ni kuwa na mgawanyo sawa wa rasilimali za nchi kwa manufaa ya kila raia na sio kwa kundi la wachache kujilimbikizia utajiri kwa njia zisozo halali.

Bi. Anne alisema ingawa uamuzi wa wabunge hao licha ya kuwa ni mgumu na utakaoleta matokeo baadaye unapaswa kuungwa mkono na kila mwananchi kwakuwa serikali imeonyesha nia ya kukabiliana na vitendo hivyo.

``Rais wa nchi ameonyesha kukerwa na hali hii ya vitendo vya wazi kwa baadhi ya viongozi... hatua hiyo inatupa moyo kwa sisi wabunge kuendelea na mapambano haya kwa ajili ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.``

``Kwa msingi huo, tunaomba wananchi watuombee ili pamoja na mambo mengine tuweze kuyafikia malengo hata kama matokeo hayataonekana sasa lakini vizazi vijavyo vishuhudie jitihada zetu``, alisema.

Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya kuwepo mgawanyiko miongoni mwa wabunge kwa kuona baadhi yetu tukihitaji mabadiliko na wengine wakipuuza.

Alisema wabunge wengi wanataka mabadiliko wakati wachache wanayapinga na kwamba wanaofanya hivyo kuhofia mabadiliko hayo yatagusa maslahi yao binafsi.

``Nasisitiza kwamba ni vyema tukawaacha hata kama wakitubeza...hatutakata tamaa kwa hili kwakuwa ni la maslahi ya wananchi na taifa``, alisema.

Katika hatua nyingine, mbunge huyo aliwataka wabunge wa CCM kuwa mstari wa mbele kukosoa viongozi wanaokiuka wajibu wa kazi kwa maslahi binafsi.

Alisema akiwa mbunge wa CCM na mjumbe wa Halmashauri Kuu hatapenda kuona chama na serikali vikitetereka.

Mbunge huyo alikuwa katika ziara ya siku mbili jimboni mwake iliyokuwa imelenga kuzindua ujenzi wa visima 30 vya maji safi katika tarafa ya Mamba Vunta pamoja na kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kusindika tangawizi ya wakulima wa kata za Mamba Miyamba, Bwambo na Mpinji.
Back to top Go down
View user profile
dRUPosts : 5
Join date : 2008-07-15

Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? Empty
PostSubject: Re: Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ?   Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? I_icon_minitimeSat Jul 19, 2008 5:51 am

Wapo waliosema "SI HASA" kwa makusudi kabisa wakiwa na maana ya kuhusisha neno SIASA. Na hata kwa kizungu wapo waliyosema "POLITRICKS" kwa mtazamo huo huo wakiwa na maana ya "POLITICS".

Katika uwanja wa Siasa huwa panakuwa na mchanganyiko mkubwa sana wa watu wa jinsia mbali mbali, taaluma mbali mbali, vyama tofauti, mikakati tofauti na mambo mengine kadha wa kadha. Cha ajabu ni kwamba wote wanakuwa na mwimbo mmoja "Tunatetea maslahi ya wananchi na kuwaletea mandeleo hao wananchi" Huu wimbo utaimbwa na wote na kila mmoja najitahidi hiyo "Single" ama "Album" yake iwe ndiye imeshika soko.

Mbinu wanazotumia ili kukidhi hayo ambayo ndiyo haki yetu akina yakhe na ndiyo maendeleo yetu, ni kukufanya sisi tuhamasike na maneno ("ambayo mara nyingi hayana vitendo") matamu ama yaliyorembwa na kila ulibwende ambao kwa kipindi kile cha "tabia ya Kinyonga" kuwa na rangi sawa na mahala alipo ili aweze kuwa ama ni mmoja wetu kwa kheri yetu sote ama kwa manufaa yake.

Maana kujibadili kwa rangi kwa kinyonga kuna maana mbili moja kwa faida yake ili apate chakula kwa urahisi anapokuwa katika "Camouflage" ama ajikinge na maadui kwa kutoonekana akiwa katika hiyo camouflage ya jumla pale alipo.!!

Sasa tabia ya wanasiasa haipishani sana na tafsiri ya kinyonga hapo juu. Huu ni wakati sasa tunatakiwa kujua ni wakati gani Kinyonga yu nasi kwa manufaa ya wote na wakati gani yu nasi kwa kujihami yeye binafsi.

Tumeanza kuwachambua mmoja mmoja, lakini si kazi rahisi hata kidogo maana inaonyesha kuwa nao vile vile wamegutuka na wanakuwa "Waangalifu" na si "Waadilifu". Wamekuwa katika makundi ambayo silaha yake ya kujikinga ni "PESA". Wana uwezo wa kuabadili haki kuwa kosa na kosa kuwa haki (hatari kubwa!!).

Pamoja na mapungufu yote ya akina Fidel Castro, Saadam Hussein n.k. lakini bado mimi ningewatumia kufundisha watu vinyonga kama ambao tunao sasa katika nchi yetu.

Nina hakika watu kama hawa "wabunge vinyonga binafsi" tusingekuwa nao na wala wasingepata fursa ya kubwabwaja kama waliyonayo hivi sasa na kutufanya kana kwamba sisi wengine hatujui kutofautisha kati ya zuri na baya ama neno la busara na la kejeli.

Waache waendelee na midomo wazi yao na tamaa zao ila wafahamu kwa sasa hivi Wananchi wa Tanzania si wale wa "ndiyo mkuu" sasa watakuhoji kabla ya yote na watataka kujua kulikoni!!!!! Shocked
Back to top Go down
View user profile
Sponsored content
Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? Empty
PostSubject: Re: Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ?   Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ? I_icon_minitime

Back to top Go down
 
Anna Kilango's Moments: Was It Real Or Was It Hypocrisy ?
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: Your first category :: POLITIKO (SIASA)-
Jump to: