Viongozi-Wananchi Connection's Community

Baraza La Maongezi Kwa Watanzania Popote Pale Walipo.
 
HomeHome  PortalPortal  CalendarCalendar  GalleryGallery  FAQFAQ  SearchSearch  MemberlistMemberlist  RegisterRegister  Log inLog in  

Share
 

 MBOWE anahusika vipi na kifo cha CHACHA WANGWE ??

Go down 
AuthorMessage
pedejeePosts : 9
Join date : 2008-07-02

MBOWE anahusika vipi na kifo cha CHACHA WANGWE ?? Empty
PostSubject: MBOWE anahusika vipi na kifo cha CHACHA WANGWE ??   MBOWE anahusika vipi na kifo cha CHACHA WANGWE ?? I_icon_minitimeWed Jul 30, 2008 10:46 am

Mwenyezi Mungu ampokee marehemu Chacha Zakayo Wangwe na ampumzishe katika makao yake ya milele.

Kwa wale wanaofuatilia mambo ya siasa nchini Tanzania sidhani kama kweli wanaweza wakashtushwa na kichwa cha habari. Kwa muda sasa kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Freeman Aikaeli Mbowe (Mwenyekiti taifa wa CHADEMA) na marehemu Chacha Wangwe. Tofauti hizi zilikuwa ni za kihoja na ikafikia hatua hadi marehemu Wangwe akasimamishwa umakamu wenyekiti taifa CHADEMA. Kusimamishwa kwake kuliungwa mkono na Zitto ambae alitamka hadharani kwamba marehemu Wangwe alikuwa hafai.

Baadhi wakauliza kiburi hiki bwana Zitto amekitolea wapi, lakini baadae maneno yakaisha. Kwa watu wanaoijua CHADEMA kiundani wanasema kwamba kulikuwa na "kila njia" ya kuhakikisha Wangwe anatolewa katika ile nafasi kutokana na tetesi kwamba alikuwa akitarajia kugombea uwenyekiti taifa CHADEMA kitu ambacho kingemuwezesha kugombania urais. Baadhi wanadai kwamba kitendo hiki Mbowe hakufurahishwa nacho, na hivyo kuanza kuzua milolongo ndani ya chama.

Kumbuka kwamba Mbowe mwaka jana alikuwa masomoni nchini Uingereza na hivyo Wangwe alishika usukani kwa kipindi hicho, lakini kabla ya kumaliza masomo Mbowe alirudi tena nchini Tanzania na kuwa mwenyekiti kama kawaida. Katika kipindi ambacho (Mbowe) alikuwa masomoni, chama kilikuwa kikiendeshwa vizuri tu, na ndipo aliposikia tetesi toka kwa watu wa karibu kwamba anaweza asiwe mwenyekiti tena, ndipo alipochukua uamuzi wa kurudi Tanzania.

Twendeni mbele na kurudi nyuma, hivi karibuni CHADEMA imekuwa ikiendeshwa na propaganda kupita kiasi hadi inafikia hatua kwamba wananchi wanaanza kupoteza imani nayo. Uozo wote ambao umo ndani ya CHADEMA ulikuwa ukitambuliwa na marehemu Wangwe, hivyo alikuwa na nia ya kusafisha chama kitu ambacho Mbowe hakufarahishwa nacho.

Uozo huo ni pamoja na mwenyekiti wake Mbowe kujitengea mapesa kwa ajili ya kampeni na matumizi yake kiofisi ambapo wakati wa chaguzi kuu taifa, wagombea wengine hukosa pesa kabisa. Lakini Mbowe alironga na waandishi na kudai kwamba yeye binafsi hujitolea pesa zake mwenyewe mfukoni mwake kuendesha chama.*Kupenda madaraka kwa gharama yoyote* ndivyo wengine husema. Pia inasemekana Mbowe ndani ya CHADEMA ana "absolute power" anaweza akasema chochote na asikilizwe.

Sasa tuachane na huo uozo, leo hii tunafahamu kwamba Chacha Wangwe hawezi kurudi tena na kuyaongelea yale yaliyokuwa yakijiri ndani ya CHADEMA na tusitegemee chochote cha maana kitachaongelewa kwa maana kwamba wale wote waliokuwa wakimpinga (kwa majina ni Zitto, Dr. Slaa, na mwenyekiti Mbowe). Sidhani kama kuna la maana litakaloongelewa na hawa watu ingawa kamwe sitoweza kupinga ushupavu na utendaji kazi zao katika siasa (yaani Zitto na Dr. Slaa) lakini katika hili suala la kifo cha Chacha Wangwe hawana chochote cha kutuambia na tukaelewa.

KWA NINI CHADEMA INATULAZIMISHA TUAMINI CHACHA WANGWE KAULIWA NA "MAFISADI" NA WAO HAWAHUSIKI
  • Hadi leo hii CHADEMA inahakikisha kwamba wananchi waamini kwamba Chacha Wangwe kauliwa na watu ambao hawahusiki na CHADEMA - kitu ambacho kinawafanya wengi wajiulize kwa nini CHADEMA inajishuku kupita kiasi na kusingizia wengine ?
    Kwa nini wanatumia sana "propaganda" kuzima moto huu wa kifo cha Chacha Wangwe ?
    • Baadhi ya forums zinazoongozwa na CHADEMA zinadai kwamba CCM wamehusika, sasa ningependa kujua, kama kweli CCM imehusika, ni hatua gani zilizochukuliwa iwapo kweli wamehusika ? au ndio kutishia mkubwa nyau ?
      Mengi yanasemwa na CHADEMA yote yakiwa katika mchakato wa kutaka madaraka, kitu ambacho wafuatiliaji mambo ya siasa wanadai kwamba kitakifanya CHADEMA kionekane kimepoteza dira
    . Je kama Wangwe kauliwa na mafisadi, kwani Mbowe nae sio fisadi ? au huu mchezo wa kila kitu, mtu fisadi ishakuwa dili tena ?


Je tushajiuliza mwenyekiti taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe anahusika namna gani na kifo cha Chacha Wangwe ? Hapa nadhani tutapata maswali mengi zaidi ya majibu. Hivi ni Mbowe huyu huyu tunayemjua sie ama ?
Back to top Go down
View user profile
rekesheiPosts : 17
Join date : 2008-06-20

MBOWE anahusika vipi na kifo cha CHACHA WANGWE ?? Empty
PostSubject: Re: MBOWE anahusika vipi na kifo cha CHACHA WANGWE ??   MBOWE anahusika vipi na kifo cha CHACHA WANGWE ?? I_icon_minitimeFri Aug 01, 2008 12:28 am

Wangwe ahofiwa kupigwa risasi familia yagoma kumzika
*Wahisi ana alama za kupigwa risasi shingoni
*Mbowe, Zitto wafanyiwa fujo msibani, wakimbilia Musoma

*Mrema, Mbatia, Lipumba wasema wataendelea kubaki


Waandishi Wetu, Tarime


NDUGU wa aliyekuwa Mbunge wa Tarime kwa tiketi Chadema wamegoma mwili wa ndugu yao kuzikwa ili kuruhu uchunguzi wa kifo chake ufanyike kutokana na hisia za wanafamilia kwamba alipigwa risasi hakufa kwa ajali ya gari kama ilivyotangazwa na vyombo vya usalama na ofisi ya Bunge.


Msemaji wa familia hiyo, Prof. Samuel Wangwe alisema kuwa kutokana na kifo hicho kuwa na mashaka mengi familia imeamua kufanya uchunguzi wa kina ili ijiridhisha na sababu za kifo cha mbunge huyo.


Akizungumza katika hadhira iliyokusanyika nyumbani kijijini Kemakorere, alisema familia imepata mashaka makubwa kutokana na mambo mengi na hasa sababu za kifo ambazo zimedaiwa kuwa ni ajali.


?Mambo mengi yamesemwa sasa kama familia tumeamua kufanya uchunguzi huru na wa kina ili kubaini sababu ya kifo cha marehemu, katika uchunguzi huu familia itatoa daktari wake na serikali,? alieleza.


Alisema kuwa familia imeamua kusitisha maziko hayo kutokana na mwili wa marehemu kubainika kuwa na jeraha ambalo wanadhani limetokana na kitu kingine na wala si ajali ya gari kama ilivyoelezwa.


Alipoulizwa na gazeti hili iwapo familia imefanya uchunguzi wa awali na kubainika kuwa kifo cha marehemu kimetokana na kushambuliwa kwa risasi, Prof Wange alisema kuwa ni kutokana na utata huo familia imeamua kufanya uchunguzi wa kina kwa kuzingatia taratibu na sheria.


?Ni kweli mwili wa maerehemu umekutwa na jeraha, lakini mimi sijaliona, na wala sijui kama ni la risasi, lakini kikubwa tunafanya uchunguzi kesho (leo) ili kuondoa utata wote huo, hii ni haki ya familia tumetaka hivyo na serikali imeridhia,? alieleza.


Kwa upande wa serikali, msemaji wa serikali Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, alisema kuwa serikali imeridhia kufanyika kwa uchunguzi huo ambapo familia itatoa wataalamu wa kufanya uchunguzi na serikali kutoa mwakilishi wake.


?Serikali imeruhusu uchunguzi huru ufanyike ambapo utahusisha daktari wao wa familia na sisi kwa upande wetu serikali tutatoa daktari pia,? alisema Wasira.


Ndugu mwingine wa marehemu, Kefa Wangwe, aliutangazia umati wa waombolezaji waliojitokeza kwa ajili ya maziko ambayo yalipangwa kufanyika jana kijijini kwao kwamba yameahirishwa ili kuruhu uchunguzi wa sababu za kifo cha marehemu.


Kefa alisema familia yao imeamua kuwa Marehemu Chacha hatazikwa hadi hapo madaktari watakapo uchunguza mwili wake na kubaini kifo cha mwanasiasa huyo kimesababishwa na nini.


Keba alisema?familia ya marehemu akiwamo kaka yake Prof. Wangwe, waliamua kuufunua jeneza na kudai kuwa kulikuwa na alama za kupigwa risasi shingoni iliyotokea mdomoni nyingine tumboni na kusababisha kifo chake.

?

Kefa ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa vipindi viwili hadi 2005 na kaka yao Prof. Wangwe, walisema mdogo wao hatazikwa kwanza hadi tume iundwe ikishirikisha familia ya marehemu, Serikali na madaktari bingwa ili kubaini kifo cha ndugu yao kwani kina utata. Mwili wa marehemu ulitarajiwa kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Mkoa Musoma ukisubiri kufanyiwa uchunguzi zaidi.


Habari ambazo timu ya waandishi wetu walioko Tarime na Kijijini kwa Wangwe walizopata kutoka ndani ya familia zilisema kuwa uchunguzi wa mwili huo ulifanywa na Dk Turwa Mrimi ambaye alibainisha kuwa mwili wa marehemu ulikuwa ukionyesha kuwa alipigwa risasi mdomoni na kutokea nyuma ya shingo, pamoja na kuwa na jeraha liloonyesha kuchomwa na kitu chenye ncha kali pajani kulia.


Kutokana na hali hiyo, ndugu walilazimika kukaa kikao na kujadiliana hatma ya hali hiyo, huku wakifanya mawasiliano kuagiza daktari mwingine zaidi.


Diwani wa Kata ya Kemambo, Agustino Neto Sasi, alithibitisha kufanyika kwa kikao hicho na kusema ?Siwezi kueleza kuhusu taarifa ya utafiti, ninachojua ni kweli daktari ameletwa na familia na mwili umefanyiwa uchunguzi sasa tungoje familia itatoa jibu.?


Uchunguzi mpya unataraijiwa kufanywa na timu ya madaktari kutoka hopitali ya Dk. Wilfred Kisuka Machage wa jimbo la Kurya, Kenya.


Prof. Wangwe alisema kuwa Dk. Mrimi ambaye anadaiwa kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu jana hakuwa daktari bingwa anayehusikana na uchunguzi, lakini kutokana na kuibuka utata familia imeamua kumpata daktari mbigwa ambaye ni mtaalamu.


Kutokana na hali hiyo, ibada ya maziko ambayo ilikuwa ianze saa 5 asubuhi ilikwama hali ikizidi kuwa tete na kusababisha wananchi kukaa vikundi wakisubiria hadi pale walipotangaziwa kwamba imeamuliwa kuzuia maziko.

?

Baadhi? ya viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, Manaibu Waziri?Gaudensia Kabaka, Dk James Wanyancha na Naibu Waziri wa Miundombinu wa Kenya na ambaye pia ni mbunge wa Kurya, Willfred Machage, na wakuu wawili wa wilaya za Kurya Magharibi na Mashariki Getonga na Ama Shamba.


Wengine waliohudhulia ni wabunge Nimrodi Mkono, Zito Kabwe,? Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman? Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia. Pia wabunge 20 ambao wamewakilisha Bunge.


Katika eneo la nyumbani ambako mwili ulikuwa umehifadhiwa, vurugu zilianza kuzuka huku vijana wakiwa na mabango ambao yanaonyesha kwamba hawaamini kwamba Wangwe amekufa kwa ajali. Mengi ya mabango hayo yalikuwa yakisema kwamba wanataka uchunguzi wa kina kuhusu kifo hicho.


Katika eneo hilo, baada ya kuwa na hisia za kifo hicho kimetokana kuuwawa kwa risasi, iliwalazimu baadhi ya viongozi wa Chadema, akiwamo Kabwe kupewa ulinzi mkali ambapo alikuwa analindwa na mabaunsa watatu.


Katika msiba huo kijijini Kemakorere ambako alizaliwa Wange, Zitto alikuwa na walinzi hao kila mara na kila alipokwenda ambao walikuwa wakimlinda na kumfuata.


Habari zilizopatikana zimeeleza kuwa kutokana na wasiwasi huo mara baada ya kufika Tarime, Zitto aliwasiliana na viongozi wa chama wilaya na Jeshi la Polisi ambapo walikaa kikao cha siri na maofisa wa polisi kuhusu suala la usalama wa viongozi.


Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Wilaya, Anderson Deogratias Chacha, alithibitisha kufika polisi, lakini alisema siyo kwa ajili ya maswala ya usalama wa Zitto wala Mbowe, bali ilikuwa ni kuwapelekea taarifa za hali ya ulinzi na jinsi walivyojipanga kama Chadema.


Alisema Chadema walipanga mkakati wa ulinzi kutokana na kubainika kuwa kuna kundi la watu wamepewa fedha kwa ajili ya kufanya vurugu. Hata hivyo, baada ya Mbowe kufika umati ulianza kusikika ukipiga kelele na kusema wanataka pia kumuua kwa vile Wangwe ameuawa na kudai Mbowe ni muhisika


Kutokana na kelele hizo, kuendelea vijana walizidi kurusha mawe na kuzuka vurugu kubwa hatua ambayo ililazimu polisi kuingia eneo hilo na kuwatawanya watu kwa lengo la kuimarisha ulinzi kwa viongozi wa chama na serikali waliokuwa huko.


Kundi kubwa la wananchi lilikuwa likipita sehemu mbalimbali huku likiimba kuwa Wangwe ni Mandela wao, wengine wakiimba, Barrack Obama
Back to top Go down
View user profile
 
MBOWE anahusika vipi na kifo cha CHACHA WANGWE ??
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
Viongozi-Wananchi Connection's Community :: Your first category :: POLITIKO (SIASA)-
Jump to: